TOC

This article is currently in the process of being translated into Kiswahili (~99% done).

Requirements:

Installing Apache webserver

Apache ndio seva ya tovuti ambayo inayohakikisha mashine yako ina uwezo wa kuzihudumia kurasa za tovuti. Unaweza kuwa hutaki kuiendesha seva ya umma katika mashine yako, lakini Apache ni nzuri katika hali ya upimaji, ni rahisi kuiweka, na inafanya vizuri sana na PHP. Apache ni programu ya bwerere, ambayo misimbo zake zinapatikana bila malipo.

Apache yaweza kupakuliwa kutoka http://httpd.apache.org/download.cgi. Kupeana kiungo ya moja kwa moja haitakua na maana, sababu Apache huwa inasasishwa kila mara. Elekea kwenye kurasa la kupakua na uchague kiungo sahihi chini ya kichwa kisemacho kitu kama "Apache HTTP Server X.X.X is the best available version". Wakati wa uandishi huu toleo la juzi kabisa lilikua 2.4.37. Kama wewe ni mtumizi wa Windows, ambaye hili funzo linadhania, thafadhali bonyeza link lisemalo "Win32 Binary (MSI Installer)". Kutumia kitayarishaji itafanya jambo nzima kuwa rahisi mno.

Baada ya kujipakulia kitayarishaji, ianzishe na ukubali masharti ya leseni n.k. Kila kitu kiwe katika hali ya kawaida hadi uifikie skrini hii:

Unaweza kuweka 'localhost' kwenye nafasi mbili za kwanza, kama nilivyofanya. Sio muhimu vile kwa kusudi letu na pia nafasi ya barua pepe sio muhimu. Vifungo vya redio ndivyo vina umuhimu zaidi kidogo - utapaswa kuamua ikiwa seva ya tovuti iwekwe kama huduma au la, ambayo itaanzishwa moja kwa moja na windows, au kama programu cha kiwango ambacho utakianzisha manually. Toleo la moja kwa moja litafanya kazi kwenye port 80,ambalo ni default ya port kwa mawasiliano ya HTTP, ilhali toleo la manual linafanya kazikwenye port nyingine, 8080 kwa kesi hii. Kama unavyo ona, nimefanya chaguo la pili . Tarakilishi changu tayari linakimbisha seva la tovuti nyingine kwenye port 80, na badala yake, ninalihitaji hili tu kwa kujaribu, kwa hivyo kuianzisha seva manually ninapoihitaji ndio bora kwangu.

Kwenye skrini ufuatao, chagua Typical halafu kisha endelea. Utajipata kwenye skrini ambapo utachagua njia ya kwenye seva itawekwa. Chaguo-msingi wa njia itafanya vizuri tu. Sasa ipitie mchawi na uwache aweke faili zinazohitajika. Ukishamaliza, unaweza kuianzisha seva kwa kuchagua -> Apache HTTP Server -> Control Apache Server -> Start Apache in Console. Kama uko na ukuta wa moto, itaweza kukuuliza kama unataka kuiziba Apache au la. Kama utataka kuwa na uwezo wa kuifikia seva yako kutoka mahali kwingine sio tu kupitia tarakilishi lako, uikubali agizo hilo.

Sasa seva yako mpya inapaswa kukimbia. Kuijaribu, iangalishe kivinjari chako kwenye http://localhost/ kama uliiweka kwenye port 80, au http://localhost:8080/ kama uliweka toleo la manual. Unapaswa uone maandishi yanayokwambia kwamba everything works fine. Pongezi, sasa upo na seva ya tovuti

Kwenye folda ambapo uliweka Apache, kawaida huwa ni kama vile C:\Program Files\Apache Software Foundation\Apache2.0\, utapata folda inayoitwa "htdocs". Hii ni muhimu sana, kwa maana itatumikia mzizi wa seva yako ya tovuti. Unaweza jaribu kuumba faili mpya, kisha halafu uifikie kupitia http://localhost:8080/jinalafaili, k.m http://localhost:8080/jaribio.html. Unaweza kuumba vijifolda pia. Tunapojaribu mambo kupitia sura za mafunzo hizi, tutazihifadhi kwenye folda ya htdocs, ili kuweza kuzifikia kupitia seva yetu ya tovuti, hivyo usisahau kuihusu wakati wowote ule.


This article has been fully translated into the following languages: Is your preferred language not on the list? Click here to help us translate this article into your language!